WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Union Saint-Gilloise katika mchezo wa Kundi E Europa League usiku wa Alhamisi Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool nchini England.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Ryan Gravenberch dakika ya 44 na Diogo Jota dakika ya 90 na ushei na kwa ushindi huo wanafikisha pointi sita na kuendelea kuongoza Kundi wakiizidi pointi mbili Toulouse ya Ufaransa baada ya wote kucheza mechi mbili.
Baada ya kichapo hicho, Union Saint-Gilloise wanabaki na pointi moja nafasi ya tatu mbele ya LASK ambayo haina pointi kufuatia kila timu kucheza mechi mbili.
Mchezo mwingine wa Kundi E Toulouse waliichapa LASK 1-0, bao pekee la beki wa Kimataifa wa Chile, Gabriel Suazo dakika ya 31 Uwanja wa Toulouse mjini Toulouse, Ufaransa.
0 comments:
Post a Comment