• HABARI MPYA

  Saturday, October 07, 2023

  MAN UNITED YATOKA NYUMA KUICHAPA BRENTFORD 2-1 'DAKIKA ZA MAJERUHI'


  WENYEJI, Manchester United wametoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Brentford FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Kiungo Mdenmark, Mathias Jensen alianza kuifungia Brentford FC dakika ya 26, kabla ya kiungo Mscotland, Scott McTominay kuifungia mabao mawili Manchester United dakika za nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida (90'+3 na 90'+7).
  Kwa ushindi huo, Manchester United inafikisha pointi 12 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Brentford FC inabaki na pointi zake saba nafasi ya 14 baada ya wote kucheza mechi nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATOKA NYUMA KUICHAPA BRENTFORD 2-1 'DAKIKA ZA MAJERUHI' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top