• HABARI MPYA

    Monday, October 09, 2023

    UKARABATI UWANJA WA MKAPA WAFIKIA ASILIMIA 95


    UKARABATI wa Awamu ya Kwanza unaoendelea katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam umefikia asilimia 95 na asilimia tano zilizobaki zinatarajiwa kukamilika ndani ya siku tano kuanzia leo.
    Akikagua ukarabati huo  leo Oktoba 9, 2023, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro @damasndumbaro_official amesema  tayari vyumba vinne vya wachezaji, sehemu ya kuchezea, vyumba vya waamuzi, afya na eneo la video za marejeo (VAR) umekamilika.
    " Tayari taa za kisasa 320 za mfumo wa LED zimefungwa na kuna huduma ya mtandao wa bure kabisa kwa ajili ya watazamaji wa mechi ambao tutauzindua kati ya tarehe 17 hadi 19 mwezi huu kabla ya mchezo wa ufunguzi wa African Football League kati ya  Timu ya Simba na Al Alhy ya nchini Misri  tarehe 20,2023 " amesema Mhe. Ndumbaro.
    Ameongeza kuwa, katika eneo la watu mashuhuri na sehemu ya wandishi wa Habari kazi iliyobakia ni ndogo ambayo itamalizika ndani ya siku hizo tano akiongeza kuwa mfumo wa sauti uwanjani tayari umerekebishwa.
    Dkt. Ndumbaro amesema kuwa Kampuni ya  Formula 360, itafunga mfumo wa matangazo kidijitali ambao utaanza kufanya kazi rasmi Oktoba 20, 2023 huku akisistiza kuwa baada ya mchezo huo, ukarabati mkubwa wa awamu ya pili utaendelea.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UKARABATI UWANJA WA MKAPA WAFIKIA ASILIMIA 95 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top