• HABARI MPYA

  Saturday, October 21, 2023

  GEITA GOLD YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA DODOMA JIJI NYANKUMBU


  WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa shule ya sekondari ya Nyanmkumbu mjini Geita.
  Mabao ya Geita Gold yamefungwa na Tariq Seif dakika ya 10 na Hassan Mahmoud dakika ya 86, wakati ya Dodoma Jiji yote yamefungwa na Hassan Mwaterema dakika ya 62 na 64.
  Kwa matokeo hayo, Geita Gold inafikisha pointi tano nafasi ya 12 na Dodoma Jiji pointi sita na inasogea nafasi ya 10 kutoka ya 12 baada ya wote kucheza mechi sita.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA DODOMA JIJI NYANKUMBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top