• HABARI MPYA

  Tuesday, October 17, 2023

  WASHINDI SANYA SANYA NA M-BET KUZAWADIWA TV, SIMU, FEDHA TASLIMU


  KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet Tanzania imezindua kampeni mpya ijulikanayo kwa jina la Sanya Sanya na M-Bet ambayo ina mwezesha mshindi kushinda fedha taslimu, simu ya mkononi na televisheni ya kisasa (“Smart TV).

  Akiuzungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jana, Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema lengo la kuanzisha  kampeni ya Sanya Sanya na M-Bet ni kuwazawdia wateja wao kuelekea kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.
  Mushi alisema kuwa wameanza kampeni mapema zaidi kwa lengo la kuwazawadia wateja wao wengi na kuweza kubadili maisha yao.
  Alisema kuwa kwa wateja wa M-Bet Tanzania wenye simu za kawaida maarufu kama ‘kitochi’, unatakiwa kutumia USSD menyu yao  kwa kupiga *149*19# na kuanza kubashiri matokea ya mechi kuanzia mbili za ligi mbalimbali duniani.
   
  Mushi alisema kuwa mbali ya kutumia USSD menyu hiyo, pia unaweza kubashiri kwa kutumia app ambayo lazima uipakue kwa watumiaji wa simu janja (smartphone).
  Alisema kuwa wateja wao watakao weka dau kuanzia Sh 5,000 na kubashiri kuanzia mechi mbili katika masoko yote ya kampuni ya M-Bet Tanzania kama Perfect 12, Normal, Dakika 45 na Multibet, watashinda zawadi ya televisheni ya kisasa (Smart TV) ambapo droo yake itafanyika kila wiki.
  “Wateja wetu ambao wataweka dau kuanzia Sh 2,000/=  mpaka Sh 4,999/=  na kubashiriki kuanzia mechi mbili wataingia kwenye droo ya kushinda simu ya mkononi na watakao bashiri kwa kuweka dau chini ya Sh 2,000/= wataingia kwenye droo ya kushinda Sh 200, 000 kila siku. Lengo letu ni kuwawezesha wateja wetu,” alisema Mushi.
  M-Bet ndiye mdhamini wa klabu ya Simba kwa udhamini wa miaka mitano mfululizo na inaendela  kutoa mamilinionea kupitia Jackpot ya Perfect12 na sasa Sanyasanya.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WASHINDI SANYA SANYA NA M-BET KUZAWADIWA TV, SIMU, FEDHA TASLIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top