• HABARI MPYA

  Sunday, October 29, 2023

  HAALAND AWAWEKA MBILI MAN U CITY YAUA SHETANI 3-0


  WENYEJI, Manchester United wamekutana na kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa mahasimu wao wa Jiji, Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao ya mabingwa hao wa England na Ulaya yamefungwa na mshambuliaji wake Mnorway, Erling Braut Haaland mawili dakika ya 26 kwa penalti na 49, huku la tatu likiwekwa nyavuni na kiungo Muingereza, Phil Walter Foden dakika ya 80.
  Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 24 sawa na Arsenal wakiwa wamefungana hadi kwa wastani wa mabao (GD) katika nafasi ya pili na tatu nyuma ya vinara, Tottenham Hotspur wenye pointi 26 baada ya wote kucheza mechi 10.
  Kwa upande wao Mashetani Wekundu baada ya kupoteza mchezo huo wa nyumbani wanabaki na pointi zao 15 za mechi 10 pia nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAALAND AWAWEKA MBILI MAN U CITY YAUA SHETANI 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top