TANZANIA imepangwa Kundi F pamoja na Morocco, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Ivory Coast.
Katika droo iliyopangwa usiku huu Jijini Abidjan, Kundi A lina wenyeji Ivory Coast, Nigeria, Equatorial Guinea na Guinea-Buissau.
Kundi B linaundwa na Misri, Ghana, Cape Verde na Msumbiji, wakati Kundi C lina Senegal, Cameroon, Guinea na The Gambia.
Kundi G linazikutanisha Algeria, Burkina Faso, Mauritania na Angola wakati E kuna Tunisia, Mali, Afrika Kusini na Namibia.
Fainali hizo zinatarajiwa kuanza Januari 13 hadi Februari 11, 2024, hii ikiwa mara ya tatu kwa Tanzania kushiriki Kihistoria baada ya 1980 Nigeria na 2019 Misri.
0 comments:
Post a Comment