• HABARI MPYA

  Friday, October 27, 2023

  KMC YAAMBULIA SARE 1-1 NA TANZANIA PRISONS UHURU


  WENYEJI, KMC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Kipa Wilbol Maseke alianza kujifunga dakika ya 53 kuipatia Tanzania Prions bao la kuongoza, kabla ya mshambuliaji Waziri Junior kuisawazishia KMC dakika ya 82.
  Kwa matokeo hayo, KMC inafikisha pointi 12, ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati Tanzania Prisons inatimiza pointi sita na kusogea nafasi ya 13 kwenye Ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YAAMBULIA SARE 1-1 NA TANZANIA PRISONS UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top