• HABARI MPYA

  Tuesday, October 10, 2023

  AUCHO, AZIZ KI NA DIARRA WAENDA KUTUMIKIA TIMU ZAO ZA TAIFA


  WACHEZAJI watatu wa kigeni Yanga SC, kipa wa Kimataifa wa Mali, Djigui Diarra na viungo Mganda Khalid Aucho na Mburkinabe Stephane Aziz Ki wamekwenda kujiunga na timu zao za taifa.
  Kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi baada ya kurejea Dar es Salaam kutoka Mwanza ambako Jumamosi waliichapa Geita Gold 3-0  katika mechi ya Ligi Kuu ya NBC Uwanja wa CCM Kirumba.
  Haijajulikana Kocha Mualgeria wa Taifa Stars, Adel Amrouche ataita wachezaji wangapi wa Yanga kwenye kikosi chake, maana sera zake kwa sasa kutotangaza kikosi katika vyombo vya Habari.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AUCHO, AZIZ KI NA DIARRA WAENDA KUTUMIKIA TIMU ZAO ZA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top