• HABARI MPYA

  Wednesday, October 25, 2023

  JKT TANZANIA YAICHAPA TABORA UNITED 1-0 CHAMAZI


  TIMU ya JKT Tanzania imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex Jijini Dar es Salaam.
  Bao pekee la JKT Tanzania ambayo Tabora United zote zimepanda Ligi Kuu msimu huu limefungwa na kiungo na Maka Edward Mwasomola dakika ya 17.
  Kwa ushindi huo, JKT Tanzania ambao ni mabingwa wa Ligi ya Championship msimu uliopita inafikisha pointi 11 na kusogea nafasi ya tano, wakati Tabora United inayobaki na pointi zake tisa inaangukia nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKT TANZANIA YAICHAPA TABORA UNITED 1-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top