• HABARI MPYA

  Friday, October 06, 2023

  FEISAL AFUNGA BAO PEKEE AZAM FC YAICHAPA COASTAL 1-0


  TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Coastal Unión katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Feisal Salum Abdallah dakika ya 45 na kwa ushindi huo Azam FC inafikisha pointi 13 katika mchezo wa tano na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ikiizidi pointi moja Simba SC ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao Coastal Unión leo wametimiza mechi tano za kucheza wakiwa na pointi mbili tu katika nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FEISAL AFUNGA BAO PEKEE AZAM FC YAICHAPA COASTAL 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top