• HABARI MPYA

    Thursday, October 19, 2023

    KAGERA SUGAR YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0 MANUNGU


    TIMU ya Kagera Sugar imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
    Mabao ya Kagera Sugar leo yamefungwa na Ally Nassor ‘Ufudu’ dakika ya 30 na Said Omar dakika ya 90.
    Kwa ushindi huo wanafikisha pointi nane na kusogea nafasi ya sita, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake mbili baada ya wote kucheza mechi sita na sasa inashika mkia kwenye Ligi ya timu 16.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0 MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top