• HABARI MPYA

  Sunday, October 22, 2023

  KAZE AAMUA KUACHIA NGAZI NAMUNGO FC


  MRUNDI Cedric Kaze amejiuzulu Ukocha Mkuu wa Namungo FC baada ya mechi sita tu za msimu kutokana na mwendendo usioridhisha katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
  Kaze anajiuzulu Namungo FC siku moja tu baada ya timu hiyo kufungwa na Singida Big Stars mabao 3-2 jana Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Anaondoka akiiacha timu ina pointi tatu tatu baada ya mechi sita ikiwa inashika nafasi ya 14 kwenye Ligi ya timu 16.
  Kaze alikuwa na msimu mzuri uliopita akiwa na vigogo, Yanga kama Kocha Msaidizi wa Mtunisia, Nasredeen Nabi wakishinda mataji ya Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) na kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAZE AAMUA KUACHIA NGAZI NAMUNGO FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top