• HABARI MPYA

  Saturday, October 28, 2023

  SIMBA SC YAICHAPA IHEFU SC 2-1 NA KUIKAMATA YANGA KWA POINTI


  TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na washambuliaji wake wa kigeni, Mkongo Jean Othos Baleke dakika ya 13 na Mzambia, Moses Phiri dakika ya 65, wakati la Ihefu SC limefungwa na Ismail Mgunda dakika ya 25.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 18 katika mchezo wa sita, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa tu wastani wa mabao na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.
  Ihefu SC kwa upande wao baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao saba za mechi saba nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA IHEFU SC 2-1 NA KUIKAMATA YANGA KWA POINTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top