• HABARI MPYA

  Monday, October 02, 2023

  MABINGWA 50 MTOKO WA KIBINGWA KUSHUHUDIA DERBY YA KARIAKOO KWA MKAPA


  KAMPENI kubwa ya Mtoko wa Kibingwa yazinduliwa rasmi  mabingwa 50 kushuhudia derby ya kariakoo katika Jukwaa la VIP A Novemba 05,2033 Kwa Mkapa.

  Rugambwa ameeleza kuwa promosheni ya mtoko wa kibingwa msimu wa 06 utakuwa wa kitofauti zaidi ambapo washiriki 50 watapata huduma za malazi ,usafiri pamoja tiketi ya VIP A kwa ajili ya kushuhudia derby hiyo huku zaidi mengine yakibaki kuwa ya surprise ili kuleta utofauti kwa mabingwa wa msimu uliopita.
  Aidha amefafanua zaidi kupitia promosheni hiyo imekuwa na muitikio mkubwa sana kutokana na washiriki wengi kutokea Mikoani.
  Akizungumza na Wanahabari Leo oktoba 02,2023  Afisa Habari wa Kampuni ya Betika  Juvenalius Rugambwa  amesema Kampuni hiyo imekuwa karibu na wateja wake kwa promosheni mbalimbali ili kuonesha jinsi gani ina wajali wateja wake na wanamichezo kwa ujumla na kufikisha wateja 300 wa promosheni ya Mtoko wa Kibingwa msimu uliopita.
  "Kama betika tunapata muitikio mkubw wakuendelea kuwepo kwa promosheni hii kutokana na washindi wengi kutokea mikoani hivyo tunapata muitikio kuwa kampuni imefika mbali zaidi na huduma zinawafikia tunapata mrejesho mzuri wa kampuni yetu kujitangaza. "
  Pia amesema mabingwa wabpromosheni hiyo watapatikana kwa  njia ya droo ambazo zitafanyika kila wiki siku ya jumanne ambapo rasmi zitaanza oktoba 10,2023  na kufikia kilele chake Oktoba 31,2023.
  "Ni rahisi mshiriki anatakiwa kuwa na vigezo vya kushiriki ni pamoja na kubeti mkeka wenye mechi kuanzia 03 na dau la kubeti liwe kuanzia shilingi 2000 au zaidi.
  Afisa Habari wa Kampuni ya Betika Juvenalius Rugambwa akizungumza na Wanahabari Leo Oktoba 02,2023 Jijini Dar es Salaam  wakati akizindua Promosheni ya Mtoko wa Kibingwa msimu wa 06 ambao utamalizika mwisho mwa mwezi oktoba mwaka huu ikijumuisha washindi 50 watakaojishindia tiketi za ndege na VIP A  kushuhudia derby ya Kariakoo Novemba mwaka huu
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MABINGWA 50 MTOKO WA KIBINGWA KUSHUHUDIA DERBY YA KARIAKOO KWA MKAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top