• HABARI MPYA

  Saturday, October 28, 2023

  EDDIE NKETIAH APIGA HAT TRICK ARSENAL YASHINDA 5-0


  WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Sheffield United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Nyota wa mchezo wa leo ni mshambuliaji Muingereza Edward ‘Eddie’ Keddar Nketiah mwenye asili ya Ghana ambaye amefunga mabao matatu dakika za 28, 50 na 58, wakati mabao mengine ya Arsenal yamefungwa na Fabio Vieira dakika ya 88 kwa penalti na Takehiro Tomiyasu dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 24 na kusogea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi mbili tu na vinara, Tottenham Hotspur, wakati Sheffield United inabaki na pointi yake moja mkiani baada ya wote kucheza mechi 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: EDDIE NKETIAH APIGA HAT TRICK ARSENAL YASHINDA 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top