• HABARI MPYA

  Sunday, October 22, 2023

  SARE ZATAWALA MECHI ZA LIGI KUU LRO MBEYA NA TABORA


  WENYEJI, Tanzania Prisons wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Beki Salum Kimenya alianza kujifunga dakika ya 42 kuipatia JKT Tanzania bao la kuongoza, kabla ya Jeremiah Juma kuisawazishia Tanzania Prisons dakika ya 70.
  Kwa matokeo hayo, JKT Tanzania inafikisha pointi nane na kusogea nafasi ya tisa, wakati Tanzania Prisons sasa ina pointi tano nafasi ya 13 kwneye Ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi sita.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo wenyeji, Tabora United wamelazimishwa sare ya bila kufungana na KMC Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Kwa matokeo hayo, Tabora United inafikisha pointi tisa na kupanda nafasi ya tano, wakati KMC imetimiza pointi 11 na kusogea nafasi ya nne baada ya wote kucheza mechi sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SARE ZATAWALA MECHI ZA LIGI KUU LRO MBEYA NA TABORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top