MABINGWA watetezi, Manchester City FC wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, BSC Young Boys katika mchezo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya jana Uwanja wa Wankdorf mjini Bern nchini Uswisi.
Mabao ya Manchester City yamefungwa na Manuel Akanji dakika ya 48 na Erling Haaland mawili, moja kwa penalti dakika ya 67 na lingine akimalizia pasi ya Rodri dakika ya 86, wakati bao pekee la BSC Young Boys limefungwa na mshambuliaji Mkongo, Meschack Elia Lina dakika ya 52.
Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi tisa kileleni, ikifuatiwa na RB Leipzig pointi sita, wakati Young Boys ina pointi moja sawa na Red Star Belgrade ya Seriba.
0 comments:
Post a Comment