Power Dynamos walitangulia kwa bao la mshambuliaji wake Mkongo, Andy Boyeli dakika ya 16, kabla ya beki Kondwani Chiboni kujifunga dakika ya 68 kuipatia Simba SC bao la kusawazisha.
Simba SC inakwenda Hatua ya 16 Bora kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya sare ya jumla ya 3-3 kufuatia sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita Uwanja wa Levy Mwanawaswa Jijini Ndola nchini Zambia.
Maana yake kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo Tanzania itakuwa na timu mbili hatua ya makundi, nyingine Yanga ambayo jana iliitoa Al Merreikh ya Sudan kwa jumla ya mabao 3-0, ikishinda 2-0 ugenini na 1-0 nyumbani, hapo hapo Azam Complex jana.
0 comments:
Post a Comment