• HABARI MPYA

  Thursday, October 26, 2023

  NYOTA WA ULAYA WAING’ARISHA TWIGA STARS KUFUZU OLIMPIKI 2024


  TIMU ya taifa ya wanawake ‘Twiga Starst’ imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili kufuzu Olimpiki ya mwakani Paris uliofanyika leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Twiga Stars yamefungwa na washambuliaji wake tegemeo, Opa Clement anayecheza Besiktas ya Uturuki kwa penalti dakika ya pili na Aisha Masaka wa BK Häcken ya Sweden dakika ya 85.
  Timu hizo zitarudiana Oktoba 31, Uwanja wa Taifa wa Gaborone na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Afrika Kusini katika Raundi ya Tatu.
  Kuna raundi ya Nne na ya Tano pia na ya mwisho na baadaye timu mbili zitaiwakilisha Afrika huko Paris.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NYOTA WA ULAYA WAING’ARISHA TWIGA STARS KUFUZU OLIMPIKI 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top