• HABARI MPYA

  Saturday, October 07, 2023

  CHELSEA YAIFUMUA BURNLEY 4-1 PALE PALE TURF MOOR


  TIMU ya Chelsea imetoka nyuma na kuichapa Burnley FC mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Turf Moor mjini Burnley.
  Mshambuliaji Mfaransa, Wilson Odobert alianza kuifungia Burnley dakika ya 15, lakini beki Mbelgiji Ameen akajifunga dakika ya 42 kuisawazishia Chelsea, kabla ya C. Palmer kufunga la pili kwa penalti ya  50, Raheem Sterling la tatu dakika ya 65 na Nicolas Jackson la nne dakika ya 74.
  Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 11 na kusogea nafasi ya 10, wakati Burnley inabaki na pointi zake nne nafasi ya 18 baada ya wote kucheza mechi nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAIFUMUA BURNLEY 4-1 PALE PALE TURF MOOR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top