• HABARI MPYA

  Sunday, October 08, 2023

  MABINTI WA TANZANIA U20 WAWAPIGA VIMWANA WA DJIBOUTI 5-0 CHAMAZI


  TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imeibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Djibouti katika mchezo wa kwanza Raundi ya Pili kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2024 Colombia leo Uwanja wa Azam Complex Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Tanzanite yamefungwa na Jamila Rajab mawili, Noela Luhala, Winfrida Gerlad na Yasinta Joseph na timu hizo zitarudiana Jumatano hapo hapo Azam Complex Djibouti akiwa mwenyeji na mshindi wa jumla atakutana na Nigeria katika Raundi ya Tatu ya mbioza Colombia 2024.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MABINTI WA TANZANIA U20 WAWAPIGA VIMWANA WA DJIBOUTI 5-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top