• HABARI MPYA

  Wednesday, October 11, 2023

  TANZANITE YASONGA MBELE KIBABE, SASA KUIVAA NIGERIA


  TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imefanikiwa kwenda Raundi ya Tatu ya mchujo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2024 Colombia baada ya ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Djibouti leo Uwanja wa Azam Complex Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Tanzanite leo yamefungwa na Jamila Rajab, Winfrida Gerard kila mmoja mawili, Diana Mnali, Zainabu Mohamed na Yasinta Mitoga kila mmoja bao moja.
  Tanzanite inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 12-0 baada ya kuichapa Djibouti 5-0 kwenye mchezo wa kwanza Oktoba 8 hapo hapo Azam Complex, siku hiyo Jamila Rajab akifunga mabao mawili tena, mengine Noela Luhala, Winfrida Gerlad na Yasinta Joseph.
  Kwa ushindi huo sasa Tanzanite itakutana na Nigeria katika Raundi ya Tatu ya mbio za Colombia 2024.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANITE YASONGA MBELE KIBABE, SASA KUIVAA NIGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top