• HABARI MPYA

  Friday, October 20, 2023

  SIMBA SC YAIKOSAKOSA AL AHLY, WATOA SARE 2-2 DAR


  WENYEJI, Simba SC wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Al Ahly ya Misri katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Soka Afrika (AFL) uliofanyika Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Al Ahly yamefungwa na Reda Slim dakika ya 45 na ushei na Mahmoud ‘Kahraba’ Soliman dakika ya 63, wakati ya Simba SC yamefungwa na Kibu Dennis dakika ya 53 na Sadio Kanoute dakika ya 59.
  Timu hizo zitarudiana Jumanne Uwanja wa Cairo International, Misri na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Petro de Luanda ya Angola na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAIKOSAKOSA AL AHLY, WATOA SARE 2-2 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top