// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AISHI MANULA YUKO TAYARI KUWAKABILI AL AHLY LIGI YA AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AISHI MANULA YUKO TAYARI KUWAKABILI AL AHLY LIGI YA AFRIKA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, October 10, 2023

    AISHI MANULA YUKO TAYARI KUWAKABILI AL AHLY LIGI YA AFRIKA


    KIPA namba moja wa Simba, Aishi Salum Manula anaweza kuwa tayari kwa mchezo wa kwanza wa Ligi ya Soka Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri wiki ijayo.
    Aishi Manula ambaye amekuwa nje tangu Aprili mwaka huu kwa pamoja na majeruhi mwingine, beki Mkongo, Henock Inonga Baka ‘Varane’ aliyeumia wiki mbili zilizopita wote sasa wapo fiti.
    Baada ya mapumziko ya siku mbili, kikosi cha Simba SC kitarejea mazoezini Alhamisi kujiandaa na michuano ya CAF African Football League wakianza na mechi mbili dhidi ya mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri Oktoba 20 Uwanja wa Benjamin Mkapa na Oktoba 24 Uwanja wa Cairo International .
    Majeruhi pekee anayebaki Simba ni mchezaji mmoja tu, kiungo Muivory Coast, Aubin Kramo Kouamé ambaye Madaktari watatazama Alhamisi kujua anaendeleaje.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AISHI MANULA YUKO TAYARI KUWAKABILI AL AHLY LIGI YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top