• HABARI MPYA

    Thursday, October 19, 2023

    MAONYESHO YA ART & HOME WEEK) KUFANYIKA MASAKI OKTOBA 25


    KAMPUNI ya Creative Option kwakushirikiana na Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) wameandaa maonesho maalum ya sanaa mbalimbali maarufu kama (Art & home Week)yatakayofanyika Wire house Masaki kuanzia tarehe 25-27 mwezi huu.
    Maonesho hayo  yanatariwa kuwakutanisha  wajasiriamali wakubwa na wadogo wa kazi za sanaa na ubunifu mbalimbali ambapo pamoja na kubadilishana uzoefu na kujenga mhusiano ya kibiashara katika kazi za sanaa na ubunifu, pia watapata fursa ya kukutana na wadau mbalimbali wa sekta hiyo kutoka katika taasisi, mashirika na makampuni mbalimbali ya ndani na nje ya nchi na kuboresha soko na kazi yasana na ubunifu.
    Akizungumzia maonesho hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika viwanja vya Wire House ambapo maonesho hayo yanatarajiwa kufanyikia, Mwakilishi wa waadaaji wa maonesho hayo bwana Japhet Ole Lengine amesema maonesho hayo yanalenga kuwakutanisha wasanii,wasanifu na wadau wengine wa sanaa ili kubadilishana uzoefu, kuongeza mtandao na kukuza soko la bidhaa zinazotokana na sanaa.
    “Sisi tumeona ni wakati mwafaka kuleta mtazamo tofauti katika kazi ya sanaa kwakuwaleta pamoja wasanii, wasanifu na wabunifu ili kuwakutanisha na wateja, wadau wa kazi zao pamoja na wapenzi wa bidhaa zinazotokana na sanaa. 
    Msemaji huyo aliongeza kuwa wadau wanaotegemewa kushiriki maonesho ya art & home week ni wasanifu majengo, wabunifu wa thamani za ndani, wauzaji wa vifaa vya ujenzi, wadau wa bima za nyumba na thamani, wadau wa umeme na wengine wanaojihusisha na mambob yanayofanana na hayo.
    Kwa upande wake mwakilishi wa baraza la sanaa Tanzania (BASATA) ambaye ni rais wa shirikisho la sanaa Tanzani Bw Adrian Nyangamalle amesema kazi ya ubunifu  na usanifu ni sehemu ya sanaa, hivyo BASATA inatambua umuhimu wa mainesho hayo na kwamba wanayatumia kama sehemu ya fursa katika kukuza na kuiongezea thamani bidhaa inayotokana na sanaa nchini “tunatumia nafasi kama hizi kuonesha kwa uma na serikali jinsi rasilimalisanaa na ubunifu inavyoshika kasi katika maendeleo yetu na kwakweli tunaomba watanzania wate watembee wajionee kazi nzuri inayofanywa na wasanii wetu”
    Aidha, baadhi ya washiriki wa maonesho hayo Fatema kutoka Empress Faniture wameyasifia maonesho na kusema sio tu yanatengeneza ajira za muda mfupi kwa watanzani wengi bali pia kuongeza dhamani ya bidhaa husika kwa kuipa nafasi ya kuinekana kupitia watu, taasisi, makampuni na mashirika mbalimbali watakaoshiriki au kudhamini maonesho hayo lakini kupitia matangazo yatakayorushwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAONYESHO YA ART & HOME WEEK) KUFANYIKA MASAKI OKTOBA 25 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top