• HABARI MPYA

  Tuesday, October 31, 2023

  TWIGA STARS YASONGA MBELE KUFUZU OLIMPIKI YA PARIS 2024


  TIMU ya taifa ya wanawake’Twiga Starst’ imefanikiwa kwenda Raundi ya Tatu ya mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za Michezo ya Olimpiki mwakani Paris baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Botswana Uwanja wa Taifa Jijini Gaborone nchini humo.
  Bao pekee la Twiga Stars leo limefungwa na mshambuliaji wa BK Häcken ya Sweden, Aisha Masaka na kwa matokeo hayo mabinti wa Tanzania wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-0 kufuatia kuilaza Botswana 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam.
  Sasa Twiga Stars itamenyana na Afrika Kusini katika Raundi ya Tatu, ambayo imeitoa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Kuna jumla raundi ya Nne za mchujo na mwishowe timu mbili za Afrika zitaiwakilisha Afrika huko Paris.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TWIGA STARS YASONGA MBELE KUFUZU OLIMPIKI YA PARIS 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top