• HABARI MPYA

  Saturday, October 21, 2023

  PAMBA FC YAICHAPA TRANSIT CAMP 2-1, KEN GOLD NA MBEYA KWANZA HAZISHIKIKI


  TIMU ya Pamba FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Transit Camp katika mchezo wa Ligi ya NBC Championship leo Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
  Mechi nyingine za Ligi ya NBC Championship, Pan African imetoa sare ya 0-0 na Mbeya City Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, Ken Gold imeifunga Cosmopolitan 2-0 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya na Mbeya Kwanza imeichapa Mbuni FC 2-1 Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha na Mbeya.
  Ligi ya NBC Championship itaendelea kesho kwa mechi mbili kupigwa, Cocpo United na Green Warriors Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza na Polisi Tanzania dhidi ya Biashara United Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
  Msimamo wa NBC Championshiop sasa ni Ken Gold pointi 16 kileleni ikiizidi tu wastani wa mabao Mbeya Kwanza na Pamba FC pointi 14 nafasi ya tatu baada ya wote kucheza mechi saba.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PAMBA FC YAICHAPA TRANSIT CAMP 2-1, KEN GOLD NA MBEYA KWANZA HAZISHIKIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top