TIMU ya Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Ladack Chassmbi dakika ya 20 na Seif Abdallah Karihe mawili, dakika ya 49 na 58, wakati la Geita Gold alijifunga kipa Mohamed Makaka dakika ya 83.
Ushindi huo wa kwanza kwa Mtibwa Sugar na wa kwanza kwa kocha Zubery Katwila tangu arejee Manungu unaifanya Mtibwa Sugar ifikishe pointi tano na kusogea nafasi ya 13, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake tano na kushukia nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi saba.
0 comments:
Post a Comment