• HABARI MPYA

  Sunday, October 29, 2023

  JOB, MAX AZIZ KI KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA YANGA


  BEKI mzawa, Dickson Nickso Job atachuana na viungo wageni, Mburkinabe Stephane Aziz Ki na Mkongo Max Mpia Nzengeli kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora klabu hiyo mwezi Oktoba.
  TAZAMA VIDEO ALLY KAMWE AKIZUNGUMZIA TUZO ZA YANGA
  Watatu hao wanaweka historia ya kuwa wachezaji wa kwanza kuwania tuzo hiyo baada ya klabu hiyo kuingia mkataba na Shirika la Bima Taifa (NIC) kudhaminizi Tuzo hizo ambazo zinaanza mwezi huu.
  Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NIC Insurance, Karim Meshack amesema mshindi wa Tuzo hiyo atazawadiwa Kiasi cha Fedha Taslimu Shilingi Milioni 4.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOB, MAX AZIZ KI KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top