• HABARI MPYA

  Sunday, October 15, 2023

  KOCHA ALIYEZIPELEKA NUSU FAINALI MERREIKH NA HILAL AFRIKA ATUA SINGIDA


  KLABU ya Singida Big Stars imemtambulisha Mbrazil, Heron Ricardo Ferreira kuwa Kocha wake mpya Mkuu akichukua nafasi ya Mjerumani, aliyedumu ofisini kwa wiki mbili tu.
  Kocha huyo mwenye umri wa miaka 65 ana uzoefu mkubwa wa kufundisha soka kuanzia nyumbani kwao mwaka 1992, Olaria ikiwa ni klabu yake ya kwanza kabla ya kufanya kazi Asía na Afrika.
  Miongoni mwa klabu alizofundisha Afrika ni pamoja na Ismailia ya Misri, Al-Ahly Shendi, Al Ahly na Al Merreikh zote za Sudan.
  Mafanikio yake makubwa barani ni kuifikisha Al Hilal Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2006-2007 na Al Al-Merreikh Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho mwaka 2012. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA ALIYEZIPELEKA NUSU FAINALI MERREIKH NA HILAL AFRIKA ATUA SINGIDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top