• HABARI MPYA

  Sunday, October 08, 2023

  PRISONS YAICHAPA MTIBWA SUGAR 3-2 SOKOINE


  TIMU ya Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Edwin Barua dakika ya 41, Joshua Nyantini dakika ya 75 na Beno Ngassa dakika ya 81, wakati ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Matheo Anthony dakika ya 19 na Kassim Hamisi dakika ya 48.
  Kwa ushindi huo, Tanzania Prisons inafikisha pointi nne na kusogea nafasi ya 13, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake mbili nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRISONS YAICHAPA MTIBWA SUGAR 3-2 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top