• HABARI MPYA

  Sunday, October 29, 2023

  LIVERPOOL YAIFUMUA NOTTINGHAM FOREST 3-0 ANFIELD


  WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Nottingham Forest katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Diogo Jota dakika ya 31, Darwin Nunez dakika ya 35 na Mohamed Salah dakika ya 77.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 23 na kusogea nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi moja na Arsenal inayoshika nafasi ya pili, wote wakiwa nyuma ya Tottenham Hotspur yenye pointi 26 baada ya wote kucheza mechi 10.
  Kwa upande wao Nottingham Forest baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 10 za mechi 10 nafasi ya 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAIFUMUA NOTTINGHAM FOREST 3-0 ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top