• HABARI MPYA

  Saturday, October 21, 2023

  MANCHESTER CITY YAICHAPA BRIGHTON & HOVE ALBION 2-1 ETIHAD


  MABINGWA watetezi, Manchester City FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na washambuliaji wake, Muargentina Julián Álvarez dakika ya saba na Mnorway, Erling Haaland dakika ya 19, wakati bao pekee la Brighton & Hove Albion limefungwa na kinda wa Hispania, mzaliwa wa Guinea-Bissau, Ansu Fati dakika ya 73.
  Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 21 na kupanda kileleni mwa ligi hiyo ikiizidi pointi moja Liverpool, wakati Brighton & Hove Albion inabaki na pointi zake 16 nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER CITY YAICHAPA BRIGHTON & HOVE ALBION 2-1 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top