• HABARI MPYA

  Thursday, October 05, 2023

  SIMBA SC YAISHINDILIA PRISONS 3-1 PALE PALE SOKOINE


  TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na kiungo Mzambia, Clatous Chotta Chama dakika ya 34, Nahodha na mshambuliaji John Bocco dakika ya 45 na ushei na kiungo Mrundi, Saido Ntibanzokiza dakika ya 86 kwa penalti, wakati la Prisons limefungwa na Edwin Barua dakika ya 12.
  Simba SC inafikisha pointi 12 na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC, ikiizidi Azam FC pointi mbili na mabingwa watetezi, Yanga pointi tatu baada ya wote kucheza mechi nne.
  Kwa upande wao Tanzania Prisons baada ya kipigo cha leo inabaki na pointi moja baada ya kucheza mechi nne ikiendelea kushika mkia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAISHINDILIA PRISONS 3-1 PALE PALE SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top