• HABARI MPYA

  Friday, October 27, 2023

  LIVERPOOL YAICHAPA TOULOUSE 5-1 EUROPA LEAGUE


  TIMU ya Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Toulouse ya Ufaransa katika mchezo wa Kundi E UEFA Europa League usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Diogo Jota dakika ya tisa, Wataru Endo dakika ya 30, Darwin Núñez dakika ya 34, Ryan Gravenberch dakika ya 65 na Mohamed Salah dakika ya 90, wakati la Toulouse limefungwa na Thijs Dallinga dakika ya 16.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi tisa na kuendelea kuongoza Kundi hilo, ikifuatiwa na Union Saint-Gilloise ya Ubelgiji na Toulouse zenye pointi nne kila moja, wakati LASK ya Austria ambayo haina pointi inashika mkia. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA TOULOUSE 5-1 EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top