• HABARI MPYA

  Saturday, October 28, 2023

  NAMUNGO FC YAICHAPA AZAM 3-1 PALE PALE CHAMAZI


  WENYEJI, Azam FC jana wamechapwa mabao 3-1 na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Namungo FC jana yamefungwa na Pius Buswita dakika ya 10, Hashim Manyanya dakika ya 19na Reliant Lusajo dakika ya 50, wakati bao pekee la Azam FC limefungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 70.
  Kwa ushindi huo, Namungo FC inafikisha pointi sita na kusogea nafasi ya 12 kwenye ligi ya timu 16, wakati Azam FC inabaki na pointi zake 13 nafasi ya tatu baada ya wote kucheza mechi saba.
    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAICHAPA AZAM 3-1 PALE PALE CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top