• HABARI MPYA

  Tuesday, October 10, 2023

  MWAKINYO AFUNGIWA MWAKA MMOJA KUPIGANA NCHINI


  BONDIA Hassan Mwakinyo amefungiwa mwaka mmoja na kutozwa Faini ya Sh. Milioni 1 baada ya kushindwa kupanda ulingoni kwenye pambano lake la Septemba 29 dhidi ya Mnamibia, Julius Indongo ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
  Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) imeona 
  sababu zilizotolewa na Mwakinyo kwa kukataa kupigana hazikuwa na mashiko.
  Hiyo inakuwa mara ya pili kwa Mwakinyo kuzua taharuki kwenye mapambano yake baada ya Septemba 3, mwaka jana kugoma kuendelea na pambano raundi ya nne akiwa anaongoza dhidi ya mwenyeji, Liam Smith ukumbi Echo Arena Jijini Liverpool.
  Kwa sababu hiyo, Bodi ya Ngumi za Kulipwa Uingereza (BBBC) ikamfungia bondia huyo kupigana nchini humo licha ya utetezi kwamba  alipoteza begi Uwanja wa Ndege ambalo lilikuwa lina vifaa vyake ikiwemo viatu.
  Mwakinyo alisema wenyeji wake walimpa viatu ambavyo vilikuwa vinambana ndio maana raundi ya nne akashindwa kuendelea kustahmilili maumivu na kujiuzulu.
  Na kuhusu pambano na Indongo, Mwakinyo alisema Promota alimhadaa na kuwashirikisha maadui zake kwenye pambano hilo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWAKINYO AFUNGIWA MWAKA MMOJA KUPIGANA NCHINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top