• HABARI MPYA

  Friday, October 06, 2023

  TABORA UNITED YAWACHAPA DODOMA JIJI FC 2-1 MWINYI


  TIMU ya Tabora United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Mabao ya Tabora United zamani Kitayosce yamefungwa na mshambuliaji Mghana, Eric Okutu dakika ya 50 kwa penalti na Abbas Athumani dakika ya 90 na ushei, wakati la Dodoma Jiji FC limefungwa na Yassin Mgaza dakika ya pili.
  Kwa ushindi huo, Tabora United inafikisha pointi nane na kupanda nafasi ya tano, wakati Dodoma Jiji FC wanabaki na pointi zao tano nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TABORA UNITED YAWACHAPA DODOMA JIJI FC 2-1 MWINYI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top