BAO pekee la Elvis Rupia dakika ya 43 limeipa Singida Big Stars ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Singida Big Stars inafikisha pointi tano na kusogea nafasi ya nane, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake mbili nafasi ya 14 baada ya wote kucheza mechi nne.
0 comments:
Post a Comment