• HABARI MPYA

  Saturday, October 14, 2023

  IHEFU SC YAACHANA NA KOCHA ZUBERI KATWILA


  KLABU ya Ihefu imeachana na Kocha wake, Zuberi Katwila baada ya takriban miaka minne ya kuwa timu hiyo tangu awasili kutoka Mtibwa Sugar.
  Taarifa ya Ihefu SC leo imesema; “Uongozi wa timu yetu umefikia makubaliano ya pande mbili ya kuvunja Mkataba na aliyekua Kocha wetu Mkuu Zuber Katwila,”.
  “Hata hivyo uongozi wa timu unamshukuru Kocha katwila kwa wakati wote aliokua nasi ndani ya timu kama Kocha Mkuu tangu alipojiunga nasi mwaka 2020,”
  “Ihefu Sc inamtakia kila la kheri Kocha Katwila katika maisha yake mapya ya soka na atabaki kuwa Mwanafamilia wa MbogoMaji,”.
  Lakini taarifa hiyo haijasema kwa wakati huu timu itakuwa chini ya nani kuelekea mechi zijazo za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU SC YAACHANA NA KOCHA ZUBERI KATWILA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top