MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wamepangwa Kundi D pamoja na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri, CR Belouizdad ya Algeria na Medeama ya Ghana katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Watani wao, Simba wapo Kundi B pamoja na Wydad Athletic ya Morocco, ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Jwaneng Galaxy ya Botswana.
Kundi A kuna Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Pyramids ya Misri, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Nouadhibou ya Mauritania.
Kundi C lenyewe linazikutanisha Esperance, Etoile Du Sahel za Tunisia, Petro Atlético ya Angola na Al Hilal ya Sudan.
0 comments:
Post a Comment