• HABARI MPYA

  Friday, October 20, 2023

  RAIS WA CAF MOTSEPE AMTEMBELEA RAIS DK SAMIA IKULU DODOMA


  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan (kulia) akipokea kumbukumbu ya zawadi ya uenyeji wa ufunguzi wa michuano ya kwanza ya Ligi ya Soka Afrika (AFL) kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe ambaye amemtembelea leo Ikulu, Chamwino Jijini Dodoma.
  Motsepe ambaye aliongozana na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), alipeleka shukrani hizo kwa Rais Samia kutokana na Tanzania kuwa mwenyeji wa ufunguzi wa michuano ya AFL inayoanza leo kwa Simba kumenyana na Al Ahly ya Misri Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS WA CAF MOTSEPE AMTEMBELEA RAIS DK SAMIA IKULU DODOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top