• HABARI MPYA

  Wednesday, October 18, 2023

  HABIB KONDO ATUPIWA VIRAGO MTIBWA SUGAR, KATWILA AREJEA MANUNGU


  KLABU ya Mtibwa Sugar imefikia makubaliano ya pande zote mbili kuachana na Kocha wake, Habib Kondo baada ya mechi tano tu za mwanzo za msimu.
  Hatua hiyo inakuja siku moja kabla ya Mtibwa Sugar kumenyana na wapinzani wao wa kutengeneza Sukari, Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
  Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar ya Bukoba kesho Saa 10:00 jioni Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro na waliokuwa makocha wasaidizi, Awadh Juma na Patrick Mwangata ndio wataiongoza timu kesho.
  Lakini taarifa za ndani zinasema kwamba aliyekuwa kocha wa Ihefu SC, Zubery Katwila yupo kwenye mazungumzo yanayoendelea vizuri na uongozi wa Mtibwa Sugar ili arejee kwneye timu hiyo aliyoichezea na kuifundisha awali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HABIB KONDO ATUPIWA VIRAGO MTIBWA SUGAR, KATWILA AREJEA MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top