KIUNGO Mkongo wa Azam FC, Yannick Bangala, amechanika msuli wa nyuma ya paja, kwenye mchezo wa jana dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Taarifa ya Azam FC imesema kwamba baada ya mechi hiyo, Bangala alirejea Dar ss Salaam kwa vipimo zaidi, wakati timu ikielekea Tanga kwa ajili ya mchezo dhidi ya Coastal Union, Oktoba 6.
“Baada ya vipimo ndiyo itajulikana ukubwa wa tatizo na muda wa matibabu hadi kupona,” imesema taarifa ya Azam FC.
0 comments:
Post a Comment