• HABARI MPYA

  Sunday, January 30, 2022

  CAMEROON NA BURKINA ZATINGA NUSU FAINALI AFCON

  WENYEJI, Cameroon wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Gambia jana Uwanja Douala.
  Mabao ya Cameroon jana yalifungwa na mshambuliaji wa Lyon ya Ufaransa, Karl Brillant Toko Ekambi yote mawili dakika ya 50 na 57 na sasa watakutana na Brukinha Faso, ambayo imeitoa Tunisia kwa kuichapa 1-0, bao pekee la Dango Ouattara dakika ya 45 na ushei Uwanja wa Roumde Adjia, Jijini Garoua. 


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAMEROON NA BURKINA ZATINGA NUSU FAINALI AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top