• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 22, 2009

  Phiri: Simba sasa mbeleeee


  KOCHA wa Simba, Mzambia Patrick Phiri, amesema baada ya kuwafunga Villa Squad mabao 2-0 juzi, kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, sasa wanachotaka ni kuendeleza wimbi lao la ushindi katika mechi zijazo, ili waweze kupanda juu katika msimamo wa Ligi Kuu ya Bara, unaoongozwa na Yanga.
  Mabao ya Simba katika ushindi wa juzi yalitiwa kimiani na mshambuliaji Mussa Hassan ‘Mgosi’ na Ulimboka Makingwe, huo ukiwa ni ushindi wa pili mfululizo tangu ilipoilaza Polisi Morogoro 3-2 Uwanja huo huo.
  Phiri aliiambia bongostaz.blogspot.com kwamba wachezaji wake wapo kwenye kiwango cha juu mno, kitu ambacho kinamuongezea matumaini ya kufanya vizuri katika mzunguko huu wa lala salama, ingawa mzunguko wa kwanza Simba haikufanya vizuri ikiwa chini ya Mbulgaria Krasmir Bezinski.
  “Hatuna cha kupoteza kwa sasa, tunachohitaji ni ushindi mnono kwa kila mechi inayokuja mbele yetu, ili tuwe katika nafasi nzuri ikiwezekana kutwaa ubingwa unaoliliwa na timu zote zinazoshiriki patashika hii ya Vodacom,” alisema kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia.
  “Najua ni kazi kubwa, lakini kutokana na uwezo wa wachezaji wangu pamoja na hasira waliyokuwa nayo, naamini tutafanikiwa, endapo wote tutakuwa na nia moja kila tutakapocheza na timu pinzani,” alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  1 maoni:

  Unknown alisema ... 23 Januari 2009 12:53

  SIJUI VIONGOZI MLIKUWA WAPI KUMCHUKUA KOCHA HUYO AU NANYI MLIWAIGA YANGA MKASAHAU CHAMWENZIO SIO CHA KWAKO,NADHANI MMEYAONA MAKOSA YENU HIVYO LAZIMA MBADILIKE JAMANI KAMA TOKA MWANZO MNGELIANZA HIVYO MNGEKUWA WAPI?

  Item Reviewed: Phiri: Simba sasa mbeleeee Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top