• HABARI MPYA

  Monday, January 24, 2022

  TANZANITE YAENDA KUWEKA KAMBI KARATU


  BAADA ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Ethiopia jana katika mchezo wa Raundi ya Tatu kufuzu Kombe la Dunia kwa wasichana chini ya umri wa miaka 20 baadaye mwaka huu nchini Costa Rica, kikosi cha Tanzanite kimeondoka leo Zanzibar kwenda Karatu kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa marudiano.
  Tanzanite ambayo bao lake pekee lilifungwa na Christian Bahera  Uwanja wa Amaan jana, imewkea katika katika hosteli za akademi ya Black Rhino mjini humo kujiandaa na mchezo wa marudiano ambao utafanyika Februari 4 Jijini Addis Ababa.


   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANITE YAENDA KUWEKA KAMBI KARATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top