• HABARI MPYA

    Saturday, April 06, 2024

    SIMBA YACHAPWA 2-0 NA AHLY CAIRO


    TIMU ya Simba SC kwa mara nyingine imetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika Hatua ya Robó Fainali baada ya kufungwa 2-0 na wenyeji, Al Ahly usiku huu Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo nchini Misri.
    Mabao yaliyoizamisha Simba leo yamefungwa na kiungo mzawa, Amr
    El Soleya dakika ya 47 akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji Mfaransa, Anthony Mbu Agogo Modeste na mshambuliaji mzawa, Mahmoud Abdelhamid Soliman dakika ya 90na ushei.
    Kwa matokeo hayo Al Ahly inakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-0 kufuatia kushinda 1-0 pia kwenye mchezo wa kwanza Ijumaa iliyopita Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Sasa Mabingwa hao watetezi, Al Ahly na watamenyana na mshindi kati ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Petro de Luanda ya Angola katika Nusu Fainali, ambao mechi ya kwanza zilitoka sare ya 0-0 Jijini Lubumbashi.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA YACHAPWA 2-0 NA AHLY CAIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top