• HABARI MPYA

  Saturday, April 06, 2024

  RAIS DK SAMIA AWAPOZA MACHUNGU YA KIPIGO SIMBA SC


  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amesema kwamba pamoja na kufungwa mabao 2-0 na Al Ahly usiku wa jana, lakini Simba SC ilipambana na juhudi zao zimeonekana.
  “Mchezo mzuri Simba. Usiku haukuwa wa ushindi lakini tumeziona juhudi na zinatupa faraja na matarajio kuwa, msimu ujao wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho la Soka Afrika mambo yatakuwa mazuri zaidi. Ahadi yetu ni kuendelea kuwaunga mkono na kuwapa motisha,”amesema Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kupitia ukurasa wake wa Instagram.
  Simba SC kwa mara nyingine imetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika Hatua ya Robó Fainali baada ya kufungwa 1-0 na wenyeji, Al Ahly usiku wa jana Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo nchini Misri.
  Mabao yaliyoizamisha Simba jana yalifungwa na kiungo Amr El Soleya dakika ya 47 akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji Mfaransa, Anthony Mbu Agogo Modeste na mshambuliaji, Mahmoud Abdelhamid Soliman dakika ya 90 na ushei.
  Kwa matokeo hayo Al Ahly inakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 2-0 kufuatia kushinda 1-0 pia kwenye mchezo wa kwanza Ijumaa iliyopita Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Sasa Mabingwa hao watetezi, Al Ahly na watamenyana na mshindi kati ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Petro de Luanda ya Angola katika Nusu Fainali, ambao mechi ya kwanza zilitoka sare ya 0-0 Jijini Lubumbashi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS DK SAMIA AWAPOZA MACHUNGU YA KIPIGO SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top